Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia amtaka Selasini amlipe fidia Sh3 bilioni

Mbatiaapoiic Data Mbatia amtaka Selasini amlipe fidia Sh3 bilioni

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgororo wa uongozi ndani ya Chama cha NCCR- Mageuzi sasa unazidi kufukuta na sasa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia, kumtaka Kaimu mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini, amlipe fidia ya Sh3 bilioni kwa kile anachodai kuwa ni kumkashfu.

Mbatia amefungua kesi hiyo dhidi ya Selasini ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la chama hicho, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akimlalamikia kumchalia jina pamoja na mambo mengine, kumtuhumu kuwa mwizi wa mali za chama.

Katika kesi hiyo namba 184/2022, Mbatia anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa tuhuma hizo alizozitoa Selasini dhidi yake ni za uwongo, imwamuru amuombe radhi hadharani na kisha amlipe fidia ya kiasi hicho cha pesa, Sh3 bilioni.

Wakili wa Mbatia, Hudson Mchau amesema jana Alhamisi, Oktoba 27, 2022, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge na kwamba imepangwa kutajwa mahakamani hapo Novemba 29, mwaka huu.

Wakili Mchau amesema kuwa Selasini alitoa tuhuma hizo dhidi ya Mbatia kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa miezi kadhaa sasa chama hicho kimekuwa katika mgogoro wa kiuongozi kati ya kambi mbili zinazopingana.

Kambi hizo ni ille inayoongozwa na Mbatia ambaye hata hivyo alishatangazwa kufukuzwa uanachama na wenzake kadhaa.

Miongoni mwa viongozi waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa makamu mwenyekiti Taifa Bara, Angelina John Mutahiwa na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Baraza la Wadhamini akiwemo aliyekuwa mwenyekiri wake, wakili Mohamed Tibanyendela.

Kambi nyingine ni ile inayoungwa mkono na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ikiongozwa na Selasini, akiwemo Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Ambar Haji Khamis, ambaye pia kwa sasa ni kaimu mwenyekiti Zanzibar, na aliyekuwa katibu mkuu, Martha Raphael Chiomba.

Mgogoro huo ulilipuka hadharani Mei 21, mwaka huu kambi ya kina Selasini inayoungwa mkon na ofisi ya Msajli wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kutangaza kumuondoa katika nafasi yake mwenyekiti Mbatia.

Septemba 6, kambi ya Mbatia kupitia kwa Mutahiwa na aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu, Hemed Msabaha Kanoni ilfungua kesi dhidi ya kambi ya Selasini.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Selasini, Ambar, Chiomba, Ameir Mshindani Ali, Susane Peter Masele, Beati A. Mpitabakana, Marti B. Mng’ong’o, Ramadhani Manyeko; Ruhwanya na Bodi ya Wadhamini kambi ya Mbatia, iliyounganishwa kama mdaiwa muhimu.

Katika kesi hiyo wadai wanaiomba mahakama hiyo iamuru kuwa mkutano wa NEC waliouitisha wadaiwa, Mei 21, 2022, na yote yaliyofanyika na kuamuriwa siku hiyo ni batili.

Wanadai kuwa kiliitishwa na watu wasio na mamlaka kwani Chiomba alishasimamishwa ukatibu mkuu, huku wakimkana Selasini kuwa si mwanachama wa NCCR-Mageuzi bali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Wanadai kuwa hata kama wangekuwa na mamlaka na kufuata maelekezo ya Katiba, bado kisingekuwa halali kwa kutokufikisha akidi kwani kati ya wajumbe 81, 43 wanadai kuwa hawakuwa na taarifa ya kikao hicho.

Pia wanaiomba mahakama hiyo iamuru kuwa wadaiwa hawana mamlaka ya kuitisha kikao chochote cha chama hicho na amri ya zuio la kudumu wadaiwa kujihusisha na vikao vyote vya chama hicho.

Hata hivyo Septemba 7, mwaka huu mmoja wa wadaiwa aliibua pingamizi dhidi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini kambi ya Mbatia kuwa si wajumbe halali.

Kufuatia hali hiyo, Mahakama ililazimika kusimamisha usikilizwaji wa kesi ya msingi ili kwanza kupata ufumbuzi wa wajumbe halali wa bodi hiyo.

Hivyo Jaji Kakolaki aliamuru upande mmoja wapo uwasilishe mahakamani maombi ili mahakama iweze kuchunguza na kuamua wajumbe wapi ni halali.

Lakini kabla ya mgogoro huo kuamuriwa, kambi ya Selasini ilitisha mkutano na kutangaza kuwavua uanachama Mbatia na wenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live