Ikiwa ni siku moja imepita tangu mkutano Mkuu wa Dharura wa Chama Cha NCCR -Mageuzi kumfuta uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, James Mbatia na kumvua uongozi Makamu Mwenyekiti, Angelina Rutairwa kwa madai ya kuhusika na ubadhirifu wa mali za chama, hii leo Mbatia amedai mkutano huo umeingilia uhuru wa mahakama kwani uamuzi huo umetoka katika kipindi ambacho shauri bado lipo mahakamani.
Ikiwa ni siku moja imepita tangu mkutano Mkuu wa Dharura wa Chama Cha NCCR -Mageuzi kumfuta uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, James Mbatia na kumvua uongozi Makamu Mwenyekiti, Angelina Rutairwa kwa madai ya kuhusika na ubadhirifu wa mali za chama, hii leo Mbatia amedai mkutano huo umeingilia uhuru wa mahakama kwani uamuzi huo umetoka katika kipindi ambacho shauri bado lipo mahakamani. Mbatia ameeleza hayo katika Mkutano wake na waandishi wa habari nje ya Hoteli ya Regency Park Dar es Salaam muda mfupi baada ya uongozi wa hotel hiyo kuzuia mkutano huo kufanyika ndani ya ukumbi wa hoteli kwa madai ya maagizo kutoka kwenye mamlaka.