Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia achaguliwa tena uenyekiti NCCR-Mageuzi

68650 Pic+mbatia

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. James Mbatia amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi kwa kipindi cha miaka mitano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Jumapili Julai 28, 2019 mkuu wa oganaizesheni na utawala wa chama hicho  Florian Mbeo amesema mbali na Mbatia, pia umefanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu.

"Kwa mujibu wa katiba  ya chama chetu ikitokea nafasi mgombea akawa mmoja huwa tunapiga kura za ndio na hapana,” amesema Mbeo akizungumzia uchaguzi huo ambapo nafasi nyingi mgombea alikuwa mmoja.

Amesema nafasi ya mwenyekiti aliwaniwa na Mbatia pekee na kuibuka na ushindi kwa kura 210 za ndio na tisa za hapana.

Mbeo amesema nafasi ya makamu mwenyekiti bara iliwaniwa na Angelina John aliyepata kura 200 za ndio na 19 za hapana.

"Makamu Mwenyekiti Zanzibar,  Ambar Hamis yeye alipata kura 213 za ndio na 3 za hapana kati ya kura 219,” am,esema Mbeo.

Pia Soma

Mbeo amesema mbali na viongozi hao, pia umefanyika uchaguzi wa wajumbe wa halmashauri kuu.

"Leo tutafanya uchaguzi wa kumpata katibu mkuu na naibu wake Bara na Zanzibar, mweka hazina Taifa pamoja na makamishna wa Mikoa 31 ambao watapeleka mapendekezo ya kuunda idara mbalimbali,” amesisitiza

Chanzo: mwananchi.co.tz