Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia: Wagombea wote wa NCCR jimbo la Vunjo wameenguliwa

Video Archive
Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kilimanjaro. Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema wanachama wa chama hicho waliochukua fomu kugombea uchaguzi wa Serikali za mitaa katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro wameenguliwa wote.

“Waliamua kufanya uteuzi na kubandika fomu za majina ya wagombea Novemba 4 badala ya Novemba 5, 2019 kama kanuni na ratiba ya uchaguzi inavyoelekeza.”

 “huwezi kuamini wagombea wetu wote jimbo la Vunjo wameenguliwa. Mchezo uliofanyika ni hatari  kwa usalama wa nchi na tayari nimeaidnikia Serikali barua ya malalamiko,” amesema Mbatia ambaye ni mbunge wa Vunjo.

Amesema walioenguliwa ni katika vijiji 60 kati ya vijiji 78 vya jimbo hilo. “Vitongoji 372 na mitaa 18 ya mamlaka ya mji mdogo wa Himo. Katika kijiji cha Komakundi eneo la Njiapanda ya Himo msimamizi msaidizi alijichanganya na kumpatia mgombea wetu fomu ya kuteuliwa na hivi sasa wanashinikiza airejeshe, agizo ambalo tumeligomea,” amesema Mbatia.

Chanzo: mwananchi.co.tz