Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia: Upinzani si uadui

68509 Mbatia+pic

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi nchini Tanzania, James Mabatia amesema upinzani si uadui bali ni fursa muhimu kwa viongozi kubadilishana fikra.

Mbunge huyo wa Vunjo ametoa kauli hiyo leo asubuhi Julai 27, 2019 katika mkutano mkuu wa  NCCR Mageuzi unaofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mimi naona wewe unataka kuongoza hivi, mimi nina mawazo mbadala ya kuweza kuboresha hili kwa ajili ya maendeleo endelevu ya watanzania  ndiyo maana ya upinzani. Kunapokuwa na changamoto ya upinzani. Taifa linaneemeka zaidi.”

“Ndiyo maana leo kutoka sakafu ya moyo wangu huu upinzani tunasema si uadui, lazima tukubaliane. Mabadiliko yote yanaanza katika mabadiliko ya kifikra,” amesema Mbatia.

Katika hatua nyingine, Mbatia ametumia jukwaa hilo kuwaomba radhi Watanzania baada ya chama hicho kuwa kimya kwa muda mrefu bila kuonyesha mbwembwe zozote.

“Tulijitafakari na tafakari yetu hadi jana kuhusu mabadiliko katika fikra. Niwe mkweli mimi sijazaliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa NCCR Mageuzi. Ningetamani kuona mwanamke ili kutekeleza kwa vitendo malengo ya kidunia,” amesema.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz