Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia: Sikujua Maalim Seif, Lipumba nao waliitwa na Magufuli-VIDEO

Video Archive
Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha NCCR- Mageuzi,  James Mbatia amesema aligundua kuwa Maalim Seif Sharif Hamad na Profesa Ibrahim Lipumba wameitwa na Rais John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam baada ya kumaliza mazungumzo na kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Amesema alibaini  Lipumba, mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ambaye ni mshauri mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo waliitwa baada ya kuona katika vyombo vya habari.

Machi 3, 2020 Rais Magufuli alikutana kwa nyakati tofauti na Maalim Seif, Lipumba na Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam na baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao wa upinzani walieleza walichozungumza na rais ikiwa ni pamoja na suala la uchaguzi huru na haki.

Mbatia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 10, 2020 alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Commucations Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na kumiliki chaneli ya MCL Digital.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia, (TCD) amesema awali walimwandikia barua Rais Magufuli wakimwomba akutane na vyama vya siasa, asasi za kiraia na madhehebu ya dini.

“Ombi letu tangu mwanzoni mwa 2018 tulihitaji meza ya mazungumzo ya pamoja. Hata juzi sikujua kama Maalim Seif ameitwa, wala sikujua kama Lipumba ameitwa sikujua kabisa. Nilikuja kusoma kwenye vyombo vya habari lakini sikujua wamezungumza nini.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Tangu tulipokutana kwenye summit ya TCD mwaka 2017 kule St Gasper Dodoma, tukaja kukutana steering committee (kamati tendaji), ombi letu la awali ni kukutana na uongozi wote, ndiyo msimamo wetu na ndicho tulichoomba,” amesema.

Amesema  kuwa baada ya Rais Magufuli kuchelewa kuwajibu, waliandika barua nyingine kuomba kumuona lakini haikujibiwa.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz