Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde awahakikishia mikopo wakulima wa nyanya

Fd9b68c4aa6b5c1abaca13bde790ac3b Mavunde awahakikishia mikopo wakulima wa nyanya

Wed, 16 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema iwapo atachaguliwa kuongoza tena jimbo hilo atahakikisha wakulima wa nyanya wanapata mikopo ya uhakika ili kuongeza tija ya uzalishaji na uchakataji wa nyanya.

Mavunde aliyasema hayo janakatika Kata ya Mpunguzi Kampeni za kuwania Ubunge wa Jimbo hilo.

Mbali na nyanya pia ameahidi kukuza zao la zabibu kwa kutafuta masoko ya uhakika na kuwawezesha wakina mama na Vijana kuchakata zabibu na kuuza mchuzi wa zabibu.

Kuhusu miundo mbinu, Mgombea huyo ambae pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira alisema atahakikisha anaboresha na kukamilisha ujenzi wa shule ya Sekondari Mpya ya Nkulabi iliyoanza kujengwa na Mbunge na Wananchi.

"Kuanza ujenzi wa shule ya Msingi Mpya eneo la Mlangwa ili kupunguza mwendo wa wanafunzi kutembea umbali mrefu," alisema Mavunde

Aidha amesema atakamilisha miundombinu ya miradi ya maji katika maeneo ya Mpunguzi B na Nkulabi.

"Nitasimamia usambazaji wa nishati ya umeme katika maeneo yaliyosalia machache,"alisema

Kuhusu michezo na sanaa amesema michezo na sanaa kwa kufadhili mashindano mbalimbali kwa lengo la kuikuza.

Chanzo: habarileo.co.tz