Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumaini mapya ya vigogo ACT-Wazalendo

48195 PIC+MATUMAINI

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vigogo wa ACT-Wazalendo wameelezea matumaini yao baada ya Maalim Seif Sharif Hamad, katibu mkuu wa zamani wa CUF na viongozi wengine waandamizi kujiunga na chama hicho hivi karibuni.

Machi 18 Maalim Seif na viongozi wengine walihamia ACT-Wazalendo ikiwa ni muda mchache baada ya Mahakama Kuu kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti wa CUF.

Maalim Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), siku hiyo alisema “Mimi na wenzangu, tumetafakari kwa kina kuhusu uamuzi wa kesi ulivyokwenda, tumeamua kutafuta jukwaa jingine la kutumia,” alisema.

Siku iliyofuata Maalim Seif aliyewahi pia kuwa waziri kiongozi, akiambatana na viongozi wenzake kadhaa walitinga katika ofisi za ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi.

Kufuatia hatua hiyo, vigogo waandamizi wa ACT-Wazalendo wamezungumza na Mwananchi wakimmwagia sifa Maalim Seif kuwa ni kiongozi mzoefu atakayekisaidia chama hicho kwa siku za usoni.

“Chama chochote cha siasa kinahitaji wanachama ili kiweze kusonga mbele. Ujio wa Maalim Seif na viongozi wenzake utaleta mchango mkubwa wa kuijenga ACT-Wazalendo,” alisema Dorothy Semu, katibu mkuu wa ACT-Wazalendo.

Semu alisema Maalim Seif ni kiongozi mzoefu kwa miaka zaidi ya 20, uzoefu wake, mawazo yake chanya na mbinu zake za kisiasa zitasaidia kuiweka ACT-Wazalendo katika medani nzuri za siasa.

“Maalim Seif ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa, kuja kwake kutasaidia kuiweka juu ACT-Wazalendo. Itasaidia chama hiki kupenya kiurahisi visiwani Zanzibar,” alisema Semu.

Semu anaungwa mkono na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Yeremia Maganja kuwa Maalim Seif ni mwanasiasa mwenye uwezo wa juu na ushawishi upande wa Tanzania bara na visiwani.



Chanzo: mwananchi.co.tz