Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Mashtaka ya Mbowe ni shambulio dhidi ya uhuru" Mnyika

Capture (600 X 304) CHADEMA yasema kesi ya Mbowe ni shambulizi la uhuru

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mnyika amesema kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ni mashambuizi ya uhuru, haki na demokrasia.

Ametoa kauli hiyo Oktoba 21, 2021 na kusisitiza kuwa Hukumu iliyosomwa na Jaji Siyani Oktoba 20, 2021 ya kupinga mapingamizi yote yaliyowasilishwa na upande wa Mbowe kuwa hayana mashiko yanatia dosari mfumo wa utoaji haki nchini.

"Niliwaambia kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya Mbowe ni shambulio dhidi ya uhuru, haki na demokrasia na niliwaasa kesi hii sio shambulio dhidi ya Mbowe na CHADEMA pekee yake, hukumu ya jana iliyosomwa na Jaji Siyani pamoja na kuitwa kuwa ni uamuzi mdogo kwenye kesi ndogo kwenye shauri dogo madhara yake hayako tu kwenye haki ya Mbowe kuminywa kwa kuendelea kuwa Gerezani leo ni siku ya 93 bali uamuzi huo umekwenda kutengeneza athari kwenye mfumo wa haki kwa Taifa letu"

"Uamuzi wa jana unatoa mwanya kwa Polisi kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika au kuna Mtu mwingine wanamtafuta, unatoa mwanya kuwashikilia Watuhumiwa zaidi ya saa nne bila kuwaandikisha maelezo, kwa wa msingi huo tu kwanza jukumu la kuipinga hukumu hii linapaswa kuwa la kila Mtanzania" Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live