Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mary Chatanda atoa somo kwa watendaji UWT

Mary Chatanda Atoa Somo Kwa Watendaji UWT Mary Chatanda atoa somo kwa watendaji UWT

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Marry Chatanda, ametoa rai kwa watendaji na viongozi wa umoja huo kuzingatia mafunzo wanayoyapata kwa lengo la kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Chatanda ametoa wito huo leo Desemba 11,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya makatibu wa UWT mikoa, wilaya na viongozi wa umoja huo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mafunzo haya yatawajengea uelewa viongozi na watendaji wa UWT katika kutekeleza majukumu yao kwa kuongeza wanachama, kutambua wapiga kura wapya na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM katika maeneo yenu,” amesema Chatanda.

Aidha, Chatanda amesesisitiza kuwa mafunzo hayo pia yatawajenga watendaji na viongozi hao kushauri Chama katika vikao vya kupanga maendeleo katika maeneo yenye uhitaji.

“Haya mafunzo yataendelea hadi kwa madiwani mpaka kwa wabunge ili kuwaimarisha utendajikazi wao katika kuelekea kwenye chaguzi,” amefafanua.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo, amesema ushirikiano wa kutosha unahitaji miongoni mwa watendaji hao katika kukiwezesha Chama kupata ushindi wa uhakika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji utakaofanyika mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Kama mnavyofahamu kutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2025, katika chaguzi hizo ili tupate ushindi wa kishindo ni muhimu kuwapatia mafunzo yatakayowawezesha mshiriki ipasavyo,” amesema Mwegelo.

Hata hivyo, Jokate ameshukuru uongozi wa UWT katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kilimanjaro, Kigoma, Kagera, Mbeya, Katavi, Geita na Ofisi ya UWT Zanzibar kwa michango yao kusaidia wananchi waliokumbwa na maafa katika Mji wa Katesh, wilayani Hanang’ mkoani Manyara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live