Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Marufuku kuhifadhi fedha za wakulima kwenye mifuko"- Katibu Mkuu CCM

Chongolo Dan Daniel Chongolo, Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM )

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuchangamka kununua mahindi kwa wakati ili kuwafanya wakulima kuendelea na shughuli zao za maendeleo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo Ruvuma wilayani Mbinga wakati akiongea na wananchi na wanachama wa chama hicho wakati wa ziara ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ambapo amesema, tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ununuzi wa mahindi hayo kwa awamu ya pili.

Chongolo amewaambia NFRA kuelekeza fedha hizo katika kazi husika kwani kazi ya fedha si kukaa mifukoni au kwenye akaunti za Taasisi, kazi yake ni kuelekea kwenye maeneo yaliyokusudiwa.

"Mwananchi amelima shamba lake kwa bidii, kavuna vizuri mazao yake anataka kutengeneza mambo yake na anataka kujipanga na pembejeo za msimu ujao wakicheleweshwa kwenye mambo ya Msingi watakuwa hawatendewi haki" Amesema Chongolo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live