Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapokezi ya Mbowe yatikisa Hai, afunga mitaa - VIDEO

Mbowe Cc Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya wananchi wa Kilimanjaro na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) kumpokea mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mbowe kwenda Hai tangu atoke gerezani Machi 4, mwaka huu ambako alikaa kwa miezi minane akikabiliwa na tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi.

Kesi hiyo ya Mbowe na wenzake watatu iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ilifutwa baada ya Mandesha Mashtaka Nchini (DPP), kupeleka hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka hayo.

Tangu alipotoka Mbowe, amekuwa akifanya mikutano mbalimbali ikiwemo kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimuita Ikulu jijini Dar es Salaam na kukubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kujenga Taifa

Katika mapokezi ya leo, shughuli mbalimbali zilisimama kwa muda wakati msafara wa Mbowe ukitoka uwanjani KIA kuelekea usawa wa Bomang'ombe ambapo wananchi walisimama kwa wingi.

Mbowe wakati anaondoka uwanja wa ndege msafara wake ulikuwa ukiongozwa na mbwa aliyekuwa ameshikiliwa na kijana mmoja.

Video kwa hisani ya Mwananchi Digital

View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live