Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapokezi ya Mbowe Tarime ni balaa!

Mbowe Musomaa Mapokezi ya Mbowe Tarime ni balaa!

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, John Mnyika na wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya chama hicho wamewasili mjini Tarime tayari kuhutubia mkutano wa hadhara unaofanyika uwanja wa Sabasaba maarufu kama Shamba la Bibi mjini Tarime.

Pamoja na Mbowe, wengine waliowasili ni Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Pambalu, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Sharifa Suleiman, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (Bazecha), Hashimu Issa Juma na mjumbe wa Kamati Kuu, John Heche ambaye ni mwenyeji wao.

Katika msafari huo, pia wamo mbunge wa zamani wa chama hicho kikuu cha upinzani akiwemo Joyce Mukya na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniphace Jacob.

Mkutano wa leo Jumatatu Januari 23 ni wa tatu tangu chama hicho kilipozindua mikutano yake jijini Mwanza Jumamosi Januari 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live