Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maombi zuio la ubunge wa kina Mdee yaanza kusikilizwa

Mdee Mak.jpeg Wabunge 19 waliovuliwa uanachama CHADEMA

Mon, 16 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza maombi ya waliokuwa wanachama wa Chadema na wabunge 19 wa Viti Maalum, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, mchana huu.

Maombi hayo ya zuio la muda la ubunge wao, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), yanatarajiwa kusikilizwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 na Jaji John Mgetta, kuanzia saa 8 mchana huu. Wanachama hao wa zamani wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 walivuliwa rasmi uanachama wa chama hicho, usiku wa kuamkia Mei 12, 2020, baada ya Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa Kati Kuu iliyowavua uanachama. Baraza Kuu la Chadema, ambalo ndilo chombo cha juu kabisa cha maamuzi ya Chadema lenye uamuzi wa mwisho katika kikao chake hicho liliunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu. Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachana Novemba 27, 2020, iliyowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama. Hata hivyo, hawakukubaliana na uamuzi huo, badala yake wamefungua maombi ya kibali cha kufungua kesi kupinga uamuzi huo wa Baraza Kuu kutupilia mali rufaa zao na kubariki uamuzi wa Kamati Kuu, kuwavua uanachama.

Sambamba na maombi hayo ya kibali cha kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama pia, wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wao. Katika maombi hayo wanaiomba mahakama hiyo iamuru hali iendelee kuwa kama ilivyo kuhusiana na ubunge wao, yaani waendelee kutambulika kuwa ni wabunge halali hadi maombi yao ya kibali yatakapoamuriwa.

Maombi hayo yanalenga kulizuia bunge na NEC mufanyia kazi uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema, hatua ambayo itawafanya wapoteze ubunge wao huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live