Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maombi kutafuta Uhuru wa mbowe yashika kasi Chadema

CHADEMA MAOMBI Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama na Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho ni cha kikuu cha Upinzani nchini, wameendelea kumsihi mungu aingilie kati kwenye Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho,Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake Halfan Bwire Hassan,Adam Hassan Kasekwa,Mohammed Abdillah Lingwenya wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi iliyopo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Kwa sasa Mbowe na Wenzake hao watatu wako Mahabusu ya Gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya Maombi hayo katibu wa Kanda ya Victoria,Zacharia Obad amesema njia pekee itakayomuweka huru Mbowe na wenzake wanaoshtakiwa kwa mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi ni maombi.

"Leo tumefika kanisani kwa ajili ya kusali misa ambayo lengo letu kwa muda mrefu toka Mwenyekiti na viongozi wengine walipokamatwa.Nia yetu mungu aingilie kati haki itendeke.Pia watanzania tuungane maana tunahitaji serikali inayotenda haki.Isibambikie kesi watu"amesema Obad.

Obad amesema kuwa wamemuomba mungu awajaalie watanzania moyo wa kupendana badala ya kuishi kwa visasi.

"Wanachama wengi wameingia kwenye misa na wengine hawakuvaa sare za chama sababu lengo sio kuvaa sare.Lengo ni namna gani watu wameguswa tumeona tulivyofanya majitoleo waumini walipiga makofi,inaonesha watanzania wanataka amani zaidi,hawataki mambo ya kubambikiana kesi .Hakuna watu wenye Hatimiliki ya Tanzania,Hatimiliki ni ya wote.

Hii sio mara ya kwanza wafuasi wa CHADEMA kufanya maombi hayo,kwani hivi karibuni wanachama Jijini Mwanza walifanya maombi maalum yaliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Evangelical Pentecostal Restoration (ERPC),Amos Hulilo.

Mbowe alikamatwa Julai 21,Jijini Mwanza alipokwenda kuhudhuria Kongamano la Katiba Mpya,kisha kuhamishiwa Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live