Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno ya Nape Nnauye baada ya Kinana kustaafu CCM

8454 DeSrwS4WAAE93AK TZW

Wed, 30 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye baada ya Abdularahman Kinana kustaafu kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kiongozi huyo alibadilisha mtazamo wao kisiasa.



Nape amesema kuwa watamuenzi daima,huku akimtaka apumzike mlezi wao asiye ana mfano.

“Pumzika Rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! TUTAKUENZI DAIMA! Cde. Kinana! Umepanda mbegu na ITAOTA!,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Naye Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “They Call you Abdul means Servant ,They call u Abdul Rahmaan Means Servant of Merciful Gracious ,But I Call u Mzee and Mwalim .Najua Umestaafu Ukatibu Mkuu na si Uwana CCM .Huu ndo Uimara wa chama chetu Kila kiongozi huondoka na kuacha Alama yake.Ila mwalim hastaafu Ualimu wake.”

Loading...
Chanzo: bongo5.com