Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo saba ziara ya Dk Bashiru Dar es Salaam

73771 Bashiru+pic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ziara ya siku mbili ya mtendaji mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally imetoa mwelekeo wa mambo saba yanayohimiza mabadiliko ya haraka ndani ya chama hicho, Serikali na kwa Watanzania licha ya mtihani mgumu katika utekelezaji wake.

Dk Bashiru aliyekuwa amebeba ujumbe wa mambo matatu ambayo ni utaifa; viapo; na uhai wa chama, alifanya ziara hiyo Jumanne na Jumatano wiki hii katika Manispaa ya Ubungo akiongozana na Kamati ya Siasa Mkoa, alitoa maelekezo mbalimbali kwa kila hoja.

Uchambuzi wa gazeti hili umebaini maeneo hayo yaliyobeba ziara hiyo ambayo baadhi huenda yakawa changamoto katika utekelezaji wake, ikiwamo wimbi la baadhi ya viongozi wa mashina kujiuzulu ili kugombea nafasi za uongozi kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24.

Mmoja kati ya makada wa chama hicho mkoani Morogoro, Robert Fransis alisema taadhari ya Dk Bashiru itaepusha mpasuko ndani ya chama licha ya ugumu wa kukubaliana na mazingira ya kutochukua fomu za kugombea, akisema hali huwa mbaya zaidi ngazi ya kamati ya siasa kuliko viongozi wa mashina.

“Msiwanyime fomu wakimbizi lakini wakichukua fomu watakuja kwenye taratibu za uchaguzi, mimi ni katibu wa kusimamia kanuni zilizopitishwa. Tunayo kanuni yetu, mtu mmoja cheo kimoja. Hii itafanya kazi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao,” alisema.

Dk Bashiru alitaja baadhi ya viongozi wa mashina katika Jimbo la Kawe wanaojiandaa kuachia nafasi ili kuchukua fomu, akiwataka kutokimbia viti wakati wa vita.

Pia Soma

Advertisement   ?
Pili, Dk Bashiru alizindua shina la wakereketwa Stop Over Kimara, akilifanya kuwa ngome ya ushindi wa Jimbo la Ubungo na shina la Mbenzi Luis, mtaa wa kwa Yusuf akilifanya ngome ya ushindi Jimbo la Kibamba katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mikataba ya kazi

Pia, alipandisha bendera za chama matawi ya Kimara B huku akikutana na changamoto ya mikataba ya ajira katika mradi wa ujenzi wa Standi Kuu ya Mabai Mbezi Luis kutoka kwa wafanyakazi, akiagiza kushughulikia.

Mikakati Uchaguzi Mkuu

Tatu ni mipango ya kuelekea uchaguzi ujazo. Majimbo yote ya Kibamba na Ubungo yako chini ya Chadema. CCM inaongoza kata tatu kati ya nane za Ubungo na mbili kati ya sita za Kibamba. Pia, CCM inaongoza kata 64 kati ya 91 za majimbo yote mawili.

Mwenyekiti wa CCM manispaa hiyo ya Ubungo, Lucas Mgonja akiahisi kuibuka na ushindi uchaguzi ujazo.

Jambo lingine linalotishia uhai wa chama katika manispaa hiyo ni taarifa za usaliti kwa baadhi ya viongozi kuvujisha siri za vikao, makundi ya kada walioangushwa kura za maoni na matawi kuhujumu chama kwa kutunza kadi badala ya kuzigawa kwa wanachama wapya.

Katibu wa chama katika manispaa hiyo, Sylvester Yaled alisema wanazitunza ili kuwezesha baadhi ya viongozi wa mashina kumpata mgombea watakayemtaka kupitia kura za maoni, zikiwamo kadi 600 zilizochukuliwa na tawi la Kwembe.

Mafuruku kwa viongozi

Ukiachana na mipango hiyo, jambo la tano kupitia ziara hiyo ni marufuku kwa kiongozi yeyote wa chama hicho kukifanya kama chombo cha kutoa hukumu kwa watumishi wa umma. Alimpongeza polisi wa Mkuranga mkoani Pwani ambaye siku za karibuni aligoma kutumia salamu ya ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi.’

Misimamo wa viongozi

Katika siku ya pili ya ziara yake, Dk Bashiru aliagiza viongozi wengine wa chama hicho kutoa misimamo yao kuhusu nafasi za uongozi kama ujasiri ulioonekana kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kutamka wazi kuwa hana mpango wa kugombea urais Zanzibar uchaguzi ujao.

Pamoja na mpango wa kuwasilisha mapendekezo ya kuboresha baadhi ya sheria zinazomgusa mwanamke, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliyeshiriki ziara hiyo alitangaza kuitisha mkutano mkubwa wa mabalozi wa CCM ili kueleza mafanikio ya Serikali.

Chanzo: mwananchi.co.tz