Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matatu kuwakutanisha Chadema Kesho

Chadema Chadema    Dar Dar (600 X 316) Mambo matatu kuwakutanisha Chadema Kesho

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inatarajia kukutana kesho Jumamosi Mei 11, 2024 katika ofisi yao kuu ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa jana Alhamisi Mei 9, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje ya Chadema, John Mrema.

Kamati hiyo inakutana kujadili mambo makuu matatu ikiwamo,kupokea taarifa ya uchaguzi katika ngazi mbalimbali za chama, kupokea taarifa ya tathimini ya maandamano ya awamu ya kwanza ya mikoa katika wiki ya maandamano na kuweka mwelekeo wa awamu ya pili ya maandamano.

Pamoja na kufanya usaili na kuteua wagombea wa nafasi za uongozi katika kanda nne za Nyasa, Serengeti, Victoria na Magharibi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live