Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matatu kumbeba Tulia Urais IPU

Tulia Cameroon (600 X 349) Mambo matatu kumbeba Tulia Urais IPU

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson leo anachuana vikali katika uchaguzi wa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), huku wachambuzi wakieleza ana nafasi nzuri ya kuibuka mshindi kutokana na uwezo, uzoefu na kuungwa mkono na makundi mbalimbali.

Uchaguzi huo unafanyika huko Luanda, nchini Angola kwa kuwashirikisha wagombea wanne wanawake wanaotoka Bara la Afrika, jambo ambalo ni la kihistoria katika Bunge hilo.

Wanaogombea nafasi ya urais wa IPU ni Dk Tulia (Tanzania), Adji Diarra Mergane Kanouté, (Senegal), Catherine Gotani Hara (Malawi) na Marwa Abdibashir Hagi (Somalia). Kwa sasa Dk Tulia ni mkuu wa kundi la siasa za Afrika ndani ya IPU (IPU African geopolitical group).

Mshindi katika uchaguzi huo atachukua nafasi inayoshikiliwa na Duarte Pacheco, ambaye ni Spika wa Ureno, aliyechaguliwa mwaka 2020 wakati wa mlipuko wa Uviko-19 na sasa anamaliza muda wake.

Rais atakayechaguliwa atakuwa wa 31 kuongoza chombo hicho kinachoundwa na maspika wa Bunge na wabunge kutoka nchi 120 duniani. Katika miaka 25 iliyopita, nafasi ya urais wa IPU imekaliwa na wabunge kutoka mataifa ya Misri, Hispania, India, Chile, Italia, Namibia, Morocco, Bangladesh, Mexico na Ureno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live