Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Samia awaonya madiwani wanaotumia mikopo kujinufaisha kisiasa

428e58a86e30d4911c66d8771a180170 Mama Samia awaonya madiwani wanaotumia mikopo kujinufaisha kisiasa

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kutumia mikopo ya halmashauri kama kitega uchumi au mtaji wa kisiasa.

Makamu ameyasema hayo leo katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano mkoani Tanga ambako anaendelea na ziara ya kikazi ya siku tano. Alisema Madiwani wamekuwa wakitumia fedha hizo kama mtaji na kujijenga hivyo ameonya fedha hizo zisitumike kisiasa.

Kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa sura ya 290 kifungu cha 37 kama kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2019 ambazo zinatumika katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa Tanzania Bara, zinataka halmashauri kutumia asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoa mikopo kwa makundi hayo maalum ambapo wanawake wanapata asilimia nne, vijana asilimia nne na walemavu asilimia mbili.

“Mmekuwa na tabia kutumia fedha hizi kujijenga kisiasa, sasa nawambieni, huko mbele ili jina lako lirudi kugombea udiwani itatokana na mfuko huu, pesa ya Magufuli hailiki, tumewafumbia macho kipindi hiki, kipindi, hatutawafumbia macho tena, nitakula na nyie sahani moja,”alisema Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

“Wananchi hii mikopo sio ya madiwani wenu, mnapopewa rudisheni sio mnachukua mnagawana na kuishia kuzilia chipsi, mrudishe ili na wengine wakopeshwe, lengo ni kujikwamua kiuchumi na si vinginevyo.” alisisitiza Samia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz