Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Biharamulo wamemchagua Robert Malulu kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine akipata kura 399 kati ya 756 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Murshid Ngeze amesema katika uchaguzi huo, Malulu alifuatiwa na Pili Mkaka aliyepata Kura 260, Anathory Choya kura 90 huku Lucas Herman akipataka Kura 0 ambapo kura halali zilikiwa 649 na zilizoharibika ni 7.
Wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo, ni Mkuu wa wilaya Biharamulo, Kemilembe Lwota anayekuwa Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa sambamba na Samira Khalifani na Gresmus.
Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi, Robert Malulu amewashukuru wajumbe kwa kumuamini kwa mara nyingine na katika kipindi kilichopita aliweza kufanya mambo mengi kwa kushirikiana na wananchama kuhakikisha wanaisimamia serikali kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Amesema, “Leo mmenipa nafasi nyingine nawaahidi sitawaangusha nitahakikisha nafanya Kazi kwa ushirikiano na Mbunge wetu Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa kama tulivyokuwa tukifanya hapo awali.”