Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makubaliano ya uendeshaji bandari yawaibua CCM Iringa

Bandari Ya Shangaiii Makubaliano ya uendeshaji bandari yawaibua CCM Iringa

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimelipongeza bunge na serikali kwa ufafanuzi mzuri uliojibu sintofahamu iliyojitokeza kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa uendeshaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na Dubai.

Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia utekelezaji wa makubaliano hayo yanayoelezwa yatakuwa na manufaa makubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Hillary Kipingi aliwatoa hofu wana Iringa akisema serikali ya chama chao haiwezi kuwaingiza mkenge katika kipindi ambacho wana mipango mingi inayolenga kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kipingi alisema CCM Mkoa wa Iringa kwa upande wake imefuatilia kwa umakini mkubwa ufafanuzi wa makubaliano hayo na mijadala katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari na kujiridhisha na dhamira ya dhati ya serikali katika kulishughulikia suala hilo kwa uwazi.

“Pamoja na uwazi, makubaliano hayo yameridhiwa na bunge kwa kuzingatia pia maoni ya wadau pamoja na wabunge wenyewe ambao tunaamini michango yao imezingatia maslai mapana ya wananchi wanaowawakilisha,” alisema.

Kipingi alizungumzia pia upotoshaji uliofanywa na baadhi ya watu kuhusu makubaliano hayo akisema; ” waliofanya hivyo waliteleza kwasababu ya haraka ya kuzungumza iliyosababishwa na hofu iliyochochewa na upotoshaji wenyewe.”

Alisema CCM ina imani mikataba itakayofuata baada ya makubaliano hayo kuridhiwa itatengenezwa kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia maslai mapana ya nchi na watu wake.

“CCM mkoa wa Iringa inasisitiza kama inavyosisitizwa na baadhi ya wabunge na wadau wa bandari wataalamu wetu wa sheria na mikataba kuwa makini katika hatua inayofuata ya kuandaa mikataba ili iwe na tija kwa nchi,” alisema.

Kwa kupitia taarifa yake aliyoitoa bungeni jana kuhusu makubaliano hayo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema ushirikiano huo unatarajiwa kuleta manufaa muhimu kwa nchi ikiwa ni pamoja na ongezeko la mapato, ajira, idadi ya meli na kufungua fursa pana kwa Tanzania kuongeza ufanisi wa bandari.

Profesa Mbarawa alisema Tanzania itapata manufaa zaidi ya 14, jambo ambalo kwa watanzania wapenda maendeleo ni muhimu wakayatazama makubaliano hayo kwa jicho hilo na kuunga mkono.

Profea Mbarawa amewatoa hofu watanzania akisema mkataba wa mradi utakaoandaliwa chini ya makubaliano hayo utapewa muda wake wa utekelezaji na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna mkataba wa miaka 100 kama ilivyodaiwa awali katika mitandao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live