Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makongoro akumbuka enzi za Ubunge Arusha

Makongoro Pc 660x400.jpeg Makongoro akumbuka enzi za Ubunge Arusha

Wed, 26 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema alichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mwaka 1995 kwa uwezo wake  si kubebwa kwa sababu ni mtoto wa rais mstaafu, Hayati Julius Nyerere.

Ameyasema hayo Mjini Babati  katika makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa.

Makongoro amesema alikuwa mkazi wa Arusha wakati huo alipochaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi cha chama cha NCCR-Mageuzi, “Arusha walikuwa wananiita Chamaa kwa sababu niliishi nao vizuri wakanichagua ili niwe mwakilishi wao na sio kama baadhi ya watu wanavyodai  kuwa nilichaguliwa kwa sababu ni mtoto wa baba wa Taifa.”

Kuhusu utendaji kazi katika Wilaya hiyo, amewataka viongozi mkoani humo kutowanyanyasa watumishi na wananchi kwa kuwa hatokubali kuona mnyonge akionewa kwenye eneo hilo.

“Wakuu wa wilaya pambaneni na migogoro ya ardhi, mfano hapa Babati nimefika na kukuta kuna mama mjane analalamikia kunyang’anywa eneo lake na watu wenye fedha kisha wanamwambia aende mahakamani,” Makongoro.

MTOTO JASIRI ANATANGAZA DW, AWASHANGAZA WENGI, ANA UWEZO WA AJABU, AJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA DUNIANI

Chanzo: millardayo.com