Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makongoro Nyerere awatoa wasiwasi CCM kuhusu Kinana

Makongoro Pc 660x400.jpeg Makongoro Nyerere

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasiwe na wasiwasi kuhusu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Abdulrahman Kinana, akisema atatekeleza majukumu yake katika misingi iliyoachwa na viongozi waliopita.

Makongoro ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 9, Aprili 2022, akizungumza katika mdahalo wa kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika Pwani, mkoani Kibaha.

“Kaka yetu hivi sasa ni makamu mwenyekiti, wako wenye wasiwasi lakini nawaambia tusiwe na wasiwasi nchi yetu iko vizuri na huyu atatuongoza vizuri, kama alivyosema Mama (Rais Samia Suluhu Hassan), nchi itaongozwa katika misingi tuliyoachiwa na waasisi wetu,” amesema Makongoro.

Makongoro ametoa kauli hiyo akizungumzia hatua ya Mzee Philip Mangula, kung’atuka katika nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, kisha nafasi yake ilichukuliwa na Kinana, aliyepitishwa kwa asilimia 100 kushika wadhifa huo na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, uliofanyika jijini Dodoma, tarehe 1 Aprili 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live