Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda kueleza utekelezaji ilani ya CCM 2015/20 Uwanja wa Uhuru

78598 Pic+makonda

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania kimeandaa mikutano maalum wa ndani kwa ajili ya kuwasomea wanachama wake utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2015/20.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Raymond Mwangwala amesema katiba ya chama hicho inamtaka kila msimamizi wa ilani hiyo kwenye ngazi husika kuwasomea wanachama kazi iliyofanyika.

Mkutano huo unafanyika leo Jumamosi Oktoba 5, 2019 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda ndiye atakayesoma utekelezaji wa ilani hiyo.

Mikutano huo umejumuisha viongozi na makada wa chama hicho kutoka wilaya tano za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Kinondoni, Temeke, Ilala, Ubungo na Kigamboni.

"Kwa hiyo hapa tunapokea utekelezaji wa kazi, lakini niseme tu kwamba kazi zilizofanyika ni nyingi na zinaonekana," amesema Mwangwala.

Amewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili uchaguzi ukifika wawe na sifa stahiki.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz