Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda atokwa machozi malalamiko ya mke ambaye mumewe ametekwa - VIDEO

Makonda Ccm Nsds Makonda atokwa machozi malalamiko ya mke ambaye mumewe ametekwa

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametokwa na machozi mara baada ya kusikia malalamiko ya Mwanamama mkazi wa Tinde Mkoani Shinyanga ya kutekewa mmewe na kudhulumiwa shamba lake tangu mwaka 2021 na hakuna haki stahiki yoyote iliyotendeka kwake.

Hayo yamejiri wakati Mwenezi Makonda aliposimama eneo la Tinde na kusikiliza kero za Wananchi hao akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.

"Mbona Polisi mnawaonea sana watu maskini, mtu ametekwa miaka mitatu iliyopita, eneo lake limechukuliwa na mtuhumiwa mnayemjua na kujengwa kiwanda lakini hamchukui hatua yoyote" Mwenezi Makonda.

"Basi kama mnashindwa kumtafuta mtu aliyetekwa, mmeshindwa hata kutenda haki kwa kumrudishia eneo lake ambalo Takukuru imethibitisha kwamba wanalimiki kihalali mjane wake? Hapana msifanye hivyo" Mwenezi Makonda.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kuitambua kesi hiyo na kubainisha kuwa Jalada la Kesi hiyo iliyofunguliwa miezi mitatu iliyopita lipo kwa Mwedesha Mashitaka Mkuu wa Serikali DPP.

Hoja hizo zimemfanya Mwenezi Makonda kushikwa na simanzi, kulia na kushindwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi wa Tinde Mkoani Shinyanga na kuahidi kufuatilia jambo hilo ili haki itendeke kwa haraka kwa Mwanamama huyo.

View this post on Instagram

A post shared by Chama Cha Mapinduzi (@ccmtanzania)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live