Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda atoa katapila 20 ujenzi wa barabara Kawe

Makonda 9131 Makonda atoa katapila 20 ujenzi wa barabara Kawe

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: Mwananchi

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda leo Januari 19, 2024 ameahidi kukabidhi katapira 20 kwa mbunge wa jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa barabara.

Makonda ametoa ahadi hiyo kutokana na wananchi wa jimbo hilo kulalamikia ubovu wa barabara, huku akiagiza katapila hizo zianze kazi mapema wiki inayokuja.

Sambamba na hilo, Makonda amempa maagizo Waziri wa Ardhi, Jerry Slaa kufika Bunju leo hii ili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi katika eneo hilo. Hii ni awamu ya pili ya ziara yake kitaifa ambapo anaangazia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Chanzo: Mwananchi