Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda ataka stendi iitwe Chongolo

Msafara Wa Makonda Wasimamishwa Ilemela Makonda ataka stendi iitwe Chongolo

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya hapo hapo Iringa ataomba jina la Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

"Hapa kuna kaka angu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya mimi nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake ..sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau mwana mafinga awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu."

Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20 Back To Back.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live