Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda ataja changamoto alizoziona mikoani

Makonda 9131 Makonda ataja changamoto alizoziona mikoani

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametaja changamoto mbalimbali walizokutana nazo kwenye ziara aliyoifanya katika mikoa 23 nchini, ikiwa ni pamoja na dhuluma iliyokithiri ambayo inawakandamiza wananchi wenye kipato cha chini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 5, 2024 jijini Dar es Salaam, Makonda ameeleza changamoto ya ukatili kwa watoto na wanawake kuwa bado ni tatizo katika baadhi ya maeneo.

Amewataka viongozi mbalimbali kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Amewasihi watendaji kuwajibika kwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana, na kwamba chama hakitasita kumtaja hadharani mtumishi yeyote atakayebainika anaichonganisha serikali na wananchi wake. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live