Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda asema wanawake wanaojifungua Dar, wengi ni wakazi wa Temeke

11431 Makonda+pic TanzaniaWeb

Sun, 15 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema idadi ya wanawake wanaojifungua katika Wilaya ya Temeke ni kubwa kuliko wilaya nyingine nne za mkoa huo.

Amesema mbali na takwimu hizo, pia katika wilaya hiyo wazazi wanaongoza kwa kuwaanzisha watoto wao shule.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 14, 2018 jijini hapa wakati akizungumzia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika mkoa huo.

Wilaya nyingine za mkoa huo ni Ubungo, Ilala, Kinondoni na Kigamboni.

Amesema kwa mwaka wanawake takribani 129, 210 hujifungua katika mkoa huo, kwamba mwaka 2018 hadi sasa waliojifungua ni 53,868 huku wengi wakiwa ni wa wilaya ya Temeke.

Kuhusu ilani ya uchaguzi, amesema katika sekta ya afya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi dhidi ya wahudumu wa afya yamepungua, jambo linaloashiria kuwa hali imeanza kuwa nzuri.

Amesema ilani ya CCM imebainisha matatizo yanayowakabili wananchi ikiwamo upungufu wa vituo vya huduma za afya, msongamano wa magonjwa, uhaba wa madaktari na wataalam, vifaa vya afya, ubovu wa miundombinu, lakini pia imetoa mbinu za kutatua.   

Amesema utekelezaji wa ilani hiyo ni pamoja na kuboreshwa miundombinu, kuongezwa kwa idadi ya madaktari na  watalam wengine wa afya na kuongeza vituo vya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz