Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda asema Tanzania hakuna chama cha upinzani

Paul Makonda 780x470 Makonda asema Tanzania hakuna chama cha upinzani

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: Mwananchi

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amedai kuwa hakuna vyama vya upinzani nchini bali watu aliowaita kuwa ni watoa taarifa.

“Taifa hili halina upinzania, Tanzania haina chama cha upinzania, Tanzania ina watoa taarifa waliojikusanya katika jina la vyama. Ukimuona anaongea siyo chama ni mtu anatoa taarifa na wakati mwingine taarifa anayoweza kuitoa inawezekana kabisa ikawa imetoka kwenye chanzo ambacho si cha ukweli au si cha uhakika lakini kwa sababu ni mtoa taarifa kazi ya chama chetu ni kusikiliza zile taarifa zao, na baada ya kushughulika na mtoa taaarifa tunashughulika na aliyesababisha hizo taarifa kutoka,"amesema Makonda.

Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Oktoba 26, 2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya mapokezi yake.

Chanzo: Mwananchi