Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda aombwa kushughulikia maafisa uhamiaji wasio waaminifu

Makona Aombwa Kushughulikia Maafisa Uhamiaji Wasio Waaminifu.jpeg Makonda aombwa kushughulikia maafisa uhamiaji wasio waaminifu

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi ameombwa kufuatilia baadhi ya watendaji wa jeshi la uhamiaji ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu.

Ombi hilo limetolewa na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi aliyehudhuria mkutano wa Mwenezi Makonda mjini Sumbawanga na kutaja kwamba biashara hiyo inafanyika zaidi kwenye mpaka wa Tunduma.

Mwananchi huyo ameeleza kwamba baadhi ya maafisa wa uhamiaji wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watu kuwaingiza kinyemela raia wa kigeni na kisha kuwafungia ndani na kudai fedha kutoka kwa ndugu wa wahusika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live