Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda amwaga machozi kumlilia aliyecharangwa mapanga kwa amri ya Mkurugenzi

Makonda Machozi.jpeg Makonda amwaga machozi kumlilia aliyecharangwa mapanga kwa amri ya Mkurugenzi

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja kati ya Wananchi wa Stalike katika Jimbo la Nsimbo kwa niaba ya wenzie amemueleza Katibu wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda kuwa Wananchi wa hapo walizuiliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Bw. Mohamed Ramadhan kuwa wasifanye shughuli zao za kilimo na eneo hilo jambo ambalo walimfikishia Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Ndugu. Jamila Kimaro ambapo mara baada ya kuwasikiliza akatoa kibali kwa kumuelekeza Mkurugenzi kuwaruhusu wananchi hao wakaendelee na shughuli zao.

Lakini kumbe, wakati huohuo Mkurugenzi akiwa anajua fika amelitoa eneo hilo kwa watu wengine bila kumjulisha Mkuu wa Wilaya, ikapelekea wananchi hao walipofika katika eneo lile wakavamiwa na watu ambao walimilikishwa eneo hilo kutoka kwa mkurugenzi ambao waliwapiga na wengine kuuwawa na wengine kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga.

Akizungumza mbele ya kadamnasi, Mwenezi Makonda amemuhoji mkurugenzi huyo kutaka kujua kama ni kweli yote yametokana na kauli zake za kuruhusu na kumficha Mkuu wa wake wa Wilaya juu ya kulitoa eneo hilo hali iliyopelekea matatizo yote kutokea ambapo Mkurugenzi alikiri na ndipo Mwenezi Makonda kumuuliza kama ni hivyo kwa nini usiandike barua ya kujiudhulu.

Aidha, Makonda amesema Rais Dkt. Samia yupo kwa ajili ya Wananchi wote na wasaidizi wake wapo akiwemo na yeye hivyo atalifikisha na akaamua kutoa posho yake yote kumkabidhi Mwananchi huyo aliyenusurika kifo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live