Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ameondoa hofu kwa wananchi wa Same kwa kuwaletea habari njema kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha dhamira yake kumtua mama ndoo kichwani inaendelea kukamilishwa kikamilifu.
Makonda amelithibitisha hilo baada ya kumpigia simu Waziri wa Maji Ndugu. Aweso wakati akizungumza na Wananchi wa Same ikiwa ni muendelezo wa ziara yake na kumtaka kutoa maelezo kuhusiana na mkakati wa serikali katika kuhakikisha kilio cha muda mrefu cha maji Wilayani Same kinafutwa machozi.
Naye, Waziri Aweso amesema kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia inatekeleza mradi wa maji wa Same - Mwanga na kubainisha kuwa maelekezo ya Rais Samia ni hadi kufikia mwezi wa 6 mwaka huu mradi uwe umekamilika ambapo amebainisha kuwa mradi huo utekelezaji wake umefikia asilimia 85% na hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Tsh Bilioni 290 na zaidi ya Vijiji 100 kunufaika na mradi huo.