Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda ampigia simu Waziri Silaa 'ufike haraka kutatua migogoro'

Makonda Ampigia Simu Silaa Makonda ampigia simu Waziri Silaa 'ufike haraka kutatua migogoro'

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amempigia simu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mhe. Jery Silaa na kumpa maelekezo ya CCM ya kumtaka kufika katika Kata ya Bunju leo Ijumaa tarehe 19 na kukutana na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Josephat Gwajima ili kufika maeneo yenye kero na changamoto za migogoro ya ardhi ili kutoa kauli itakayoleta utatuzi wa migogoro hiyo.

Naye Waziri Silaa amekiri kupoke agizo hilo na kulitekeleza haraka iwezekanvyo.

Mwenezi Makonda amesema ni muhimu kutatua migogoro hiyo ilikusudi Watanzania kuendelea kuona namna gani Serikali ya CCM ilivyosikivh na inatatua matatizo yao jambo litakalopelekea kuendele kuwa na Amani na Chama Cha Mapinduzi kwani uwepo migogoro hiyo inawanyima Amani na Utulivu kitu ambacho chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakihitajiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live