Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda ampa miezi 6 Majaliwa, amgeukia Jerry Silaa

#LIVE: Makonda Anaunguruma Dodoma Makonda ampa miezi 6 Majaliwa, amgeukia Jerry Silaa

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amempa miezi sita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atatue migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi.

Makonda ametoa agizo hilo leo tarehe 1 Novemba 2023, akizungumza na wananchi wa Jiji la Dodoma.

Mbali na agizo hilo kwa Waziri Majaliwa, Makonda amempa miezi miwili Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaa, kuhakikisha anatafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo.

“Chama kinamuelekeza waziri mkuu kusimamia kikamilifu suala la kutatua migogoro kwa kuunganisha wizara tatu, ardhi, maliasili na TAMISEMI. Chama kinamtaka waziri Majaliwa ndani ya miezi sita awe amesimamia na kuratibu kikamilifu kuondoa na kufuta migogoro ya ardhi,” amesema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda amemtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo jijini Dodoma, akisema asilimia 49 ya wananchi wake hawapati maji safi na salama.

Katika hatua nyingine, Makonda amewataka wapinzani huku akiwataja, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu, kama wana kero zao waziwasilishe CCM ili zifanyiwe kazi.

“Vyama vya watoa taarifa wasisite wanapokuwa na jambo lolote lile ambalo wanaliona chama tawala linaweza kulifanyia kazi, sababu sote tunajenga nyumba moja na Rais wetu anataka nchi kue. Watoa taarifa mnavyokuwa na taarifa mahususi kaka angu Lissu, Lema na Mbowe, hata kama mimi mnaogopa kunipa taarifa kuna wazee wafikishieni na tutaliangalia,” amesema Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live