Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda akagua utekelezaji wa agizo la kufungua kliniki

Makonda Akagua Utekelezaji Wa Agizo La Kufungua Kliniki.jpeg Makonda akagua utekelezaji wa agizo la kufungua kliniki

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametembelea na kukagua utekelezaji wa Agizo la CCM kuwataka Manispaa ya Iringa kufungua kliniki endelevu ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Agizo ambalo alilitoa jana tarehe 8 Februari, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Iringa Mjini.

"Ombi langu kwa watendaji muwasikilize wazee, wazazi, kaka na dada zetu kwa upendo na ndio uwe msukumo wa kwanza kwakuwa hata kama kuna mapungufu upendo una tabia ya kuyafupisha hayo mapungufu na hata kama hana haki na ukimueleza vizuri basi upendo utamfanya aondoke kwa furaha." Alisena Makonda.

"Mimi hapa mnavyoniona nalala usingizi mzuri kwa sababu moyoni mwangu sina hela na sijabeba mzigo wa mtu," alisema Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live