Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Ukistaafu, tulia na familia yako

Makonda Makondaaaa.png Makonda: Ukistaafu, tulia na familia yako

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amesema sio utaratibu kwa Wastaafu kila siku kuongeaongea huku akiwashauri Wastaafu wakishapumzika watulie na walee Familia zao na kwamba kama watahitajika kwa ajili ya kazi wataitwa.

Akiongea Jijini Dodoma leo Makonda amesema “Kuna tofauti kubwa kati ya tuliokuja Mjini kwa kuungaunga na wale tuliowakuta Mjini, tuliokuja kwa kuungaunga tumepigana vita mapori mengi sana, ndio maana hata ukiulizwa hivi Makonda ni nani hata Baba yake humjui kwasababu tumepiga vita vingi sana, niwaombe tu mliopo ndani ya CCM na nje ya CCM huyu Dkt. Samia ndiye Rais wetu ameletwa na Mungu kwa mapenzi yake Mungu tumpe nafasi ya kufanya kazi”

“Sikuweza kusema kipindi cha miaka yote ile kwasababu sikuwa na nafasi yoyote na Mimi utaratibu wangu ukipewa nafasi unapewa kazi uliyopewa ukimaliza unapumzika, huwezi kupewa kazi umemaliza umepumzika wewe ni Mstaafu lakini kila siku upo kwenye microphone, huo sio utaratibu”

“Ukishaitwa Mstaafu tulia lea Familia yako wakikuona wa maana watakuita kama walivyomuita Makonda, huwezi kuwa Mstaafu halafu kutwaa, aah, aah, na Wastaafu Nchi hii wanaheshimika sana na Mimi nimejifunza kutoka kwao, nakumbuka Marehemu Mzee Mkapa alipostaafu siku moja nimeenda nyumbani kwake nikamuuliza Mzee vipi mbona uko kimya sana akasema unataka nifanye nini?, nikamwambia Mzee unajua akasema hapana Mimi nimemaliza wajibu wangu”

“Kwahiyo tumuache Rais Samia afanye kazi , tusilipelipe Watu mitandaoni wamtukane, kama una pesa kuna Bodaboda wanahitaji pikipiki, Mamantilie wanahitaji mitaji, Wavuvi wanataka boti, kama unawapenda wape hao badala ya kuwapa Watu hela wamtukane Rais wetu na ndio maana waliposikia Makonda ameteuliwa wamepiga kelele nyingi kwasababu wanajua nawajua na hofu yao ni kuwajua, walitamani waendelee kukaa kwenye maficho wasijulikane lakini Mungu ni mwema ninawafahamu”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live