Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Ningekuwa mwenezi kipindi cha Magufuli, hao jamaa wangenyooka

Makonda Ampigia Simu Silaa Paul Makonda.

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema yeye ni Mwenezi anayebadilika kutokana na Mazingira na kama angeteuliwa katika nafasi hiyo wakati Rais akiwa Hayati John Magufuli, basi wale jamaa wangenyooka

Makonda ametoa kauli hizo akiwa katika ziara za Kichama Wilayani Moshi jana Jumatatu, Januari 22, 2023.

"Mimi ni Mwenezi ninaebadilika kutokana na mazingira, ningeteuliwa kuwa Mwenezi kipindi cha Magufuli chuma wale jamaa wangenyooka.

"Sasa Kipindi hiki na mimi najaribu kuwa na kauli za mama, Mama mstaarabu, unatamani kupiga panch lakini unasema mhhh, mama sio mapigo yake haya. Sasa kwa upendo huo kwanini tumuonee mama wa watu? Kwanini tuchafue heshima ya Taifa hili?

"Kwanini na sisi ttuwe Taifa la Maandamano kama wenzetu Wakenya mpaka wanakosa watalii?" Ameyasema Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live