Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema alinusurika ajali mara tatu kwenye ziara yake ya kuzunguka mikoa mbalimbali nchini, alipokuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza leo mjini Arusha wakati wa mapokezi yake na makabidhiano ya ofisi, Makonda amesema alinusurika kwenye ajali hizo kwa sababu ya maombi ya wananch, hivyo sasa amehamia Arusha na kwamba moto wake unaendelea kama alivyokuwa Idara ya Uenezi CCM.
Amesema wazee wa dini pamoja na mila wamekuwa wakimuombea, ana imani kubwa kwamba atawatumikia vyema wananchi wa Arusha na atatembelea wilaya zote za mkoa huo kutatua kero zao ili wananchi wapate maendeleo.