Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Ni wakati wa kusikiliza kero sio kutoa Hotuba

Paul Makonda Njombeeeee Makonda: Ni wakati wa kusikiliza kero sio kutoa Hotuba

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa, Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Paul Makonda amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)ni chama ambacho kinataka kihangaike na kero za wananchi na sio kutoa hotuba ni wakati wa kushughulikia maisha ya wananchi ambao wanachangamoto mbalimbali zinazowakabili.

Makonda amesema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani hapa ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za mikoa 20 katika kusikiliza kero za wananchi.

“Uwe wakati wa chama kiwe na faraja kwa wananchi na matumaini ya kuishi na chama hiki kimeshashinda dora hivyo hakuna sababu ya kusubiri uchaguzi kwasababu kina wajibu wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake” amesema Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live