Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makao makuu ACT-Wazalendo kuitwa jina la Maalim Seif

Malim Seif Makao makuu ACT-Wazalendo kuitwa jina la Maalim Seif

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Chama cha ACT- Wazalendo, kimeazimia masuala nane ikiwemo jengo la ofisi ya makao makuu ya chama hicho kuitwa jina la Maalim Seif Sharif Hamad ili kuenzi mchango wake.

Maalim Seif alikuwa mwenyekiti wa chama hicho ambaye alifariki dunia Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa anapatiwa matibabu.

Kwa sasa nafasi hiyo inashikikiwa na Juma Duni Haji baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika wa chama hicho Julai 2021.

Akizungumza leo Jumatatu, Septemba 5,2022, Janeth Joel Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho amesema wameridhia ofisi hiyo iliyopo Magomeni kuitwa jina hilo baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa ofisi hiyo kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar.

"Jana tulikuwa na kikao cha halmashauri kuu, pamoja na mambo mengine, iliazimia juu ya masuala mbalimbali ya ndani ya chama na ya kitaifa, ikiwemo Ofisi ya Makao Makuu (iliyopo Magomeni, Dar es Salaam) kupewa jina la Jengo la Maalim Seif kumuenzi marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa mwenyekiti wa chama chetu," amesema

Amesema kwakuwa ofisi hiyo haijakamilika, halimashauri hiyo imeielekeza sekretarieti kuwa uzinduzi wa ofisi mpya ya makao makuu uandaliwe na kufanyika mapema iwezekanavyo.

Pia halmashauri kuu hiyo imepongeza hatua iliyofikiwa sasa ya kupatikana kwa ofisi ya wasemaji wa kisekta (iliyopo Oysterbay, Dar es salaam) ambayo itawarahisishia kutekeleza majukumu yako kwenye ofisi hizo.

Maazimio mengine ni uchaguzi wa ndani ya chama, halmashauri hiyo imepitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kwa ngazi za matawi, kata, majimbo, mikoa na taifa ambao utafanyika kuanzia Machi 2023 hadi Machi 2024.

Imeipongeza kamati ya wasemaji wa kisekta kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasemea Watanzania na kuiagiza kamati hiyo kuendelea kupaza sauti katika maeneo mahsusi ya kukithiri kwa tozo za Serikali, uvunjifu wa haki za binadamu magerezani, changamoto za bima ya afya na umuhimu wa hifadhi ya jamii,imepitisha azimio la kuundwa kwa Kitengo cha chama cha kusimamia uwajibikaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (Government Oversight Unit).

Chanzo: Mwananchi