Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla: Tumesikiliza kero 148

Amos Makalla CCM Makalla: Tumesikiliza kero 148

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Amos Makalla amesema katika ziara waliyofanya kwenye Mikoa mitano hadi sasa akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi wamefanikiwa kusikiliza kero 148 za Wananchi mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi.

Akiongea leo akiwa Mkoani Njombe, Makalla amesema “Tumesikiliza kero 148 na kuzipatia ufumbuzi, niwaombe Viongozi CCM, wakati Viongozi na Watendaji wa Serikali wakifanya kazi ya kusikiliza kero na sisi Wana CCM na Wananchi wana imani kubwa na Chama chetu, kila Kiongozi katika ngazi yake tusiachie Serikali tu, wapokeeni, wasikilizeni, pelekeni mambo yanayotakiwa kutatuliwa ndani ya Serikali”

Viongozi hao wanatarajia kuikamilisha ziara yao hiyo ya Mikoa sita kesho katika Mkoa wa Songea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live