Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makada wengine CHADEMA wawekwa ndani

Chadema.jfif Chadema yadai makada wake kumi kukamatwa.

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Viongozi na wanachama wa Chadema wapatao kumi wanadaiwa kukamatwa na polisi Mkoa wa Ilala wakati wakiendelea na kikao cha ndani katika Jimbo la Segerea.

Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Baraka Mwago amesema makada hao walikamatwa jana jioni wakati wakiendelea na kikao cha ndani katika jimbo la Segerea.

Amesema katika jimbo hilo kuna operesheni ya Chadema Digital inayoendelea na walikamatwa wakiwa kwenye kiao cha kawaida.

“Polisi walivamia kwenye kikao cha ndani wakituhumu kuwa tunapanga kuhamasisha maandamano, kitu ambacho si kweli, kwenye jimbo hilo kuna operesheni ya Chadema Digital inayoendelea,”amesema Mwago.

Amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni pamoja na Julius Mwita, Gerva Lyenda, Alex Massaba, Omar Mkama, Aisha Macha, Fatuma Thabit, Patrick Asenga, Jacob Bailemba, Deogratius Kajula na Abdallah Senkamba.

Juzi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro alitoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kitakachojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyorasmi kabla na kesho wakati wa kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Chanzo: Mwananchi