Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majimbo 2 ya Temeke CUF yapitisha wagombea ubunge

1b487b92c3603143865d1813ae90ce26.jpeg Majimbo 2 ya Temeke CUF yapitisha wagombea ubunge

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam wa Chama cha Wananchi (CUF), wamepitisha majina mawili ya wagombea ubunge kupitia chama hicho ambapo mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa CUF, Abdul Kambaya amepitishwa kuwania ubunge Mbagala na Zainabu Mndolwa kuwania ubunge Jimbo la Temeke.

Aidha, wajumbe kama hao mkoani Mtwara walipitisha majina mawili ya wagombea kuwania ubunge katika jimbo la Mtwara Mjini ambapo Matfah Nachuma alipitishwa kuwania jimbo hilo na Shamsia Aziz akipita kuwania Jimbo la Mtwara Vijijini.

Akizungumza na Habari- LEO jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano, Mohamed Ngulangwa alisema hayo ni baadhi ya matokeo yanayoendelea kutolewa kwenye vikao vya wajumbe wa mikutano tofauti inayofanywa sasa ya kuwapata wagombea ubunge wa CUF.

“Uchaguzi unaendelea, wajumbe kwenye maeneo huku wilayani wanaendelea na upigaji kura kuwapata wagombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali, Temeke wamepitisha Zainab una Mbagala wamempitisha Kambaya,”alisema Ngulangwa.

Wengine waliopitishwa ni Magdalena Sakaya, anayegombea ubunge katika Jimbo la Kaliua mkoani Tabora ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bara. Akizungumza na gazeti hili, Sakaya alisema hivi sasa vikao vya mikutano ya kuwapitisha wagombea vinaendelea kwenye maeneo tofauti na kwamba kura hizo za maoni zimesogezwa muda kutoka Julai 23 hadi Julai 31,mwaka huu ili kutoa nafasi ya kuwapata wagombea kutokana na idadi ya waliotia nia kuongezeka.

“Tuko wiki ya pili sasa ya vikao vya kura za maoni kwenye wilaya kuketi kuchagua wagombea na tumeshawapata kwenye baadhi ya majimbo na kazi inaendelea, leo(jana) tulitegemea kupata majina ya walioshinda kwenye wilaya ya Tabora mjini na Kilwa.

Wakati CUF wakiendelea na harakati hizo, Chama cha Demorasia na Maendeleo (Chadema) kimeendelea kupokea fomu za wanaorejesha walioomba kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kwa chama hicho.

Katika nafasi hiyo ya urais, jumla ya watia nia 11 walijitokeza baadhi yao ni Gaspar Mwanalyela, Peter Msigwa, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe , Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lisu, Lazaro Nyalandu , Dk Maurose Majinge.

Waliorejesha fomu hizo jana ni Pamoja na Dk Mayrose na Gaspar Mwanalyela ambao walirejesha fomu zao jana baada ya kukidhi matakwa ya kikanuni na fomu zao kupokelewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi,Reginald Munisi.

Chanzo: habarileo.co.tz