Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahanga asema alishinda ubunge akiwa CCM kwa kuiba kura

13865 Pic+mahanga TanzaniaWeb

Sat, 25 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga amesema wakati akiwa CCM alishinda ubunge kwa wizi wa kura.

Dk Mahanga ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na mbunge wa Ukonga na Segerea ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 25, 2018 katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za Chadema jimbo la Ukonga.

Amesema aliweza kuwa mbunge wa Ukonga kwa miaka 10 na sababu kubwa ilikuwa kununua kura hivyo wananchi wasikubali kununuliwa.

"CCM nawafahamu sana wanawatumia mabalozi kununua kadi za kupigia kura hata mimi walikuwa wananifanyia hivyo na ninashinda,” amesema.

"Kura zinazoibiwa sio za Chadema ni za wananchi, wananchi kataeni kuibiwa.”

Uchaguzi huo mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Mwita Waitara kujiuzulu uanachama na kuhamia CCM.

Wakati CCM ikimpitisha tena Waitara kuwania ubunge Ukonga, Chadema wamempitisha Asia Msangi.

Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema),  John Heche akizungumza katika mkutano huo amesema anaijua hofu waliyonayo CCM kwa sasa.

“Najua hofu iliyopo upande wa pili kwa mimi kuja Ukonga. Niseme wazi nitakuwa kwenye kampeni hizi kuanzia leo hadi siku ya mwisho. Sababu kubwa ni kulinda heshima ya wakurya na watu wa Mara,” amesema.

Amesema kwa miaka yote Wakurya wameshiriki katika ukombozi kwa kupigania haki.

“Lakini kwa mara ya kwanza tumeaibisha nchi hii tumeaibisha Wakurya na watu wa Mara. Nipo hapa kumfundisha yule aliyetuaibisha,”amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz