Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli kuzindua chuo cha CCM Kibaha

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha.  Rais John Magufuli leo Jumatatu Julai 16, 2018 atazindua ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Viongozi mbalimbali wa chama tawala na Serikali wameshiriki uzinduzi huo, wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama vya ANC (Afrika Kusini),  Swapo (Namibia),  MPLA ( Zimbabwe), Frelimo (Msumbiji) na ZANU-PF.

Uzinduzi huo pia utashuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC),  Song Tao.

Akizungumza leo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  Humphrey Polepole amesema chuo hicho kitakuwa kikiwaandaa viongozi na kuwapika makada wa chama hicho na vyama vingine vilivyoshiriki harakati za ukombozi kusini mwa bara la Afrika.

“Hiki ni chuo cha CCM chenye lengo la kuwanoa viongozi wa chama kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa hiyo tunatarajia darasa la mwanzo kabisa kuanza  2020 kitakapokamilika,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz