Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli awataka CCM kufanya mageuzi jimbo la Mch. Msigwa

20747 Msigwa+pic Magufuli awataka CCM kufanya mageuzi jimbo la Mch. Msigwa

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewataka wanachama wa chama hicho mkoani Iringa, kuhakikisha wanafanya mageuzi kwa Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu.

Magufuli alitoa agizo hilo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, aliyekuwa akifanya mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani humo.

Jimbo la Iringa mjini linaongozwa na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.

Magufuli akizungumza na wanafunzi hao kwa njia ya simu alisema: "Nasema CCM hoyee kwa kuwa mpo Iringa nasema kamwene, basi nawashukuru sana vijana, endeleeni kuchapa kazi, ni mwaka wenu na Mungu awajalie sana endeleeni kukitetea Chama Cha Mapinduzi, ninawapenda vijana na Mungu awasaidie sana katika kuchapa kazi na ninyi ndio mnaleta jeuli ya Chama Cha Mapinduzi."

Magufuli alisema anafurahi Umoja wa Vijana wa CCM Iringa wanavyofanya kazi nzuri, hivyo ni matumaini yake wataendelea kufanya kazi na hata kuhakikisha jimbo hilo la Iringa mjini linarejea mikononi mwa CCM kwenye uchaguzi mkuu.

"Mpo kwenye Jimbo la Iringa kwa wapinzani na nitafurahi kuona vijana wa UVCCM Iringa wanafanya kazi nzuri, nimepata taarifa zao asanteni sana,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumza na vijana, Polepole alisema kuwa muda wa mbunge Msigwa kuendelea kwenda bungeni umekwisha, sasa ajiandae kwenda kusimamia mashamba yake ya nyanya na kanisa lake kwani ubunge wa jimbo hilo ameshapoteza.

Alisema kutokana na Msigwa kujua wazi kuwa jimbo hilo si lake tena, ameamua kukimbilia kuchukua fomu ya urais Chadema, nafasi ambayo hata hivyo hawezi kuipata kwani imani ya Watanzania kwa miaka mitano ijayo ni Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Polepole alikabidhi bajaji 10 zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya ahadi yake aliyokuwa ameitoa kwa vijana hao kupewa mkopo nafuu wa bajaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live