Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli arusha dongo gizani

Magu?fit=800%2C500 Magufuli arusha dongo gizani

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: dar24.com

Mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, amerusha dongo gizani kwa mmoja wa wagombea kutokea Singida ambaye hakumtaja jina akiwa katika mkutano wake wa kampeni Ikungi, mkoani Singida leo Septemba 1,2020.

“Mmoja wa Wagombea nafikiri anatoka hapa (Singida) mshaurini kwamba mimi mnipe kura nyingi nitamtafutia kikazi kidogokidogo Serikalini, ni Mtoto wetu tunampenda, mimi sina tatizo na Mtu yeyote, kwani kazi lazima uwe Rais?, akija mwambieni kwamba Magufuli amesema atakupa kazi” amesema Magufuli akiwa Ikungi Mkoani Singida.

“Mgombea anayetoka hapa (Singida) ni Mtoto wetu tunampenda, mimi sina tatizo na Mtu, Urais muachie Magufuli wewe tutakupa kikazi utakachoweza kufanyafanya, sisi wote ni wamoja, akija mwambieni Magufuli amesema atakupa kazi, kwanini unahangaikia hii kazi ambayo hutoshinda!?” ameongeza Magufuli.

Magufuli aanza rasmi Kampeni

Chanzo: dar24.com