Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema katika uongozi wake hataki kuona chama hicho tawala nchini Tanzania kinaendelea kuwa ombaomba na kuwategemea matajiri wachache.
Amesema hilo litawezekana endapo watumishi wa chama hicho wataendelea kufanya kazi na kukusanya mapato yanayotokana na miradi ya chama hicho ili waweze kuendesha vyema shughuli za chama.
Amesema matajiri lengo lao ni kukimiliki chama na kukiweka mifukoni jambo ambalo si zuri kwa maendeleo ya CCM.
Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 24, 2020 katika mkutano na viongozi wa wilaya ya mikoa wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
“Niwapongeze mnafanya kazi nzuri tukiendelea hivi mapato ya chama chetu yataendelea kuongezeka kwa kasi na tutaweza kugharamia shughuli mbalimbali ikiwemo kampeni za uchaguzi mkuu ujao.”
“Hatutaki kuona chama kinaendelea kuwa ombaomba na kuwategemea matajiri wachache ambao baadaye wanajimilikisha chama na kukiwe mifukoni mwao,” amesema Magufuli.
Pia Soma
- VIDEO: Magufuli aonya viongozi kupitisha wagombea wao uchaguzi 2020
- Magufuli ataka viongozi CCM kuitetea, kuisimamia Serikali
- Madiwani watatu wa Chadema Arusha wahamia CCM
- DC Sabaya azungumzia uchunguzi wa awali kuwasafisha wanaodaiwa kuhujumu reli